EPL YASOGEZWA MPAKA APRIL 30,2020 KWA SABABU YA CORONA
Chama cha soka cha England FA kimetangaza kuzisimamisha ligi zote za nchini humo mpaka April 30,2020 kutokana na virusi vya Corona
Vilabu vya ligi kuu nchini England vimeshiriki mkutano wa chama hicho kwa njia ya simu na kufikia maamuzi hayo ya kusimamisha ligi mpaka tarehe hiyo.
Wiki jana ilitangaza ligi kuu ya England itasimama mpaka April 4, lakini kwa sasa imeonekana jana hilo bado ni kubwa kupambana nalo, hivyo kufikia maamuzi ya kuirudisha ligi Aprili 30.
UEFA iliamua kuahirisha michuano ya Euro 2020 na kuipeleka 2021 ili kuruhusu ligi za ndani kupata muda wa kumaliza ligi zao
Mechi ya mwisho kucheza katika ligi kuu nchini England msimu huu ilikuwa ni Leicester City walipoifunga Aston Villa Machi 9.
Na mechi ya kwanza kuahirishwa katika ligi hiyo kutokana na virusi vya Corona ni Man City dhidi ya Arsenal iliyokuwa ipigwe Jumatano iliyopita. Baadae Ijumaa ligi yote ikasimamishwa baada ya kocha wa Arsenal Mikel Arteta na winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo.
Mpaka ligi inaenda kizuizini,Liverpool wapo juu kwa tofauti ya pointi 25, wakihitaji ushindi wa mechi mbili tu kutangazwa mabingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30