MSHAMBULIAJI WA REAL MADRID AOMBA RADHI KUKIUKA SHERIA ZA KUIKWEPA CORONA
Mshambuliaji wa Real Madrid na Serbia Luka Jovic ameomba radhi kufuatia kukikuka taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kujikinga na kuzuia kusambaza virusi vya corona.
Jovic ameomba radhi baada ya waziri mkuu wa taifa lake la Serbia Ana Brnabic kumkosoa vikali kwa kitendo chake cha kushindwa kukaa quarantine (chini ya uangalizi ukiwa umejitenga ili ijulikane kama ua virusi au la).
Akihojiwa na Marca Jovic alinukuliwa alisema kuwa “Madrid nilifanya vipimo vya COVID-19 na kukutwa hasi (sina virusi hivyo) ndio maana nikaamua kusafiri kwenda Serbia kuwaunga mkono watu wangu na kuwa karibu na familia kwa ruhusa ya klabu yangu”