MAN UNITED KUWALIPA MASHABIKI WAKE KWA AJILI YA CORONA
Klabu ya Man United inataraji kumlipa Pauni 350 (Tsh Milioni 1) kila shabiki aliyenunua tiketi ya mechi yao ya Europa League ya ugenini dhidi ya timu ya LASK ya Austria, ambapo kwa ujumla ni Pauni 245,000 (Tsh Milioni 708) kwa mashabiki 700 walionunua tiketi.
Maamuzi hayo yanakuja baada ya mchezo huo utakaochezwa leo kuthibitishwa kuwa utachezwa bila ya mashabiki kwa sababu ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona.
Malipo hayo yatafanywa kupitia kadi zao mashabiki walizotumia kununulia tiketi, malipo yatafanywa katika siku tano zijazo.
Corona imezidi kuathiri sekta ya michezo, ligi ya Hispania leo imetangazwa kusimama kwa muda wa wiki mbili zikiwa zimepita siku chache tangu matukio yote ya michezo kusimamishwa nchini Italia mpaka April 3.
Pia Ligi ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani NBA imesimamishwa kwa ajili ya kujilinda na virusi vya Corona.