RONALDO ABAKI URENO KUJILINDA NA CORONA
Klabu ya Juventus imethibitisha nyota wao Cristiano Ronaldo ataendelea kubakia mjini kwao Madeira,Ureno kwa kipindi hiki ambacho kuna mlipuko wa maambukizi ya Virusi vya Corona.
Cristiano aliondoka Italia kwenda Madeira Jumatatu hii Machi 9 kwa ajili ya kumuona mama yake ambaye ni mgonjwa na pia kusheherekea siku ya kuzaliwa ya dada yake.
Habari hii Juventus wanaitoa baada ya beki wao Daniel Rugani kugundulika na kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Pia wiki hii kamati ya Olimpiki ya Taifa Italia ilitangaza kusimamisha shughuli zote za michezo nchini humo mpaka April 3 kwa ajili ya kujilinda na maambukizi ya virusi Corona