SIMEONE AMFANANISHA OBLAK NA MESSI
“Kipa wetu ni bora Duniani. Anaamua mchezo kama vile Messi anavyofanya kwa Barcelona” — Haya ni maneni ya kocha wa Atletico Madrid Diego Pablo Simeone baada ya kuwatupa nje mabingwa watetezi wa michuano ya klabu Bingwa Ulaya Liverpool.
Usiku wa jana Liverpool watamkumbuka Jan Oblak,kuliko Marcos Llorente ambaye aliwafunga goli mbili.
Jan Oblak ndiye aliyeibuka nyota wa mchezo huo, akiokoa michomo mingi ya hatari na kuwanyima majogoo kwenda robo fainali ya michuano hiyo.
Mchezo huo uliisha kwa Atletico Madrid kushinda kwa goli 3-2, na kufuzu robo fainali kwa jumla ya goli 4-2 kufuatia kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Wanda Metropolitano jijini Madrid