CORONA YAFANYA FORMULAR 1 KUAHIRISHWA CHINA
Formular 1 wametangaza kuahirisha kufanyika kwa Chinese Grand Prix iliyopangwa kufanyika April 16-18 kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona nchini China.
Maamuzi hayo yamekuwa kwa ajili ya kujali afya na usalama wa madereva, wafanyakazi na mashabiki.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Formular 1 Ross Brawn amesema kuwa wataangalia kama mbio hizo zinaweza kurejea baadae mwaka huu.