AJ AMPA SHAVU FURY DHIDI YA WILDER
Bondia wa Uingereza Anthony Joshua amesema anaamini Muingereza mwezake bondia Tyson Fury atashinda pambano lake la marudiano na Deontay Wilder litakalopigwa Las Vegas Februari 22.
AJ akihojiwa na kituo cha Sky Sports kuhusu marudiano ya Tyson Fury na Deontay Wilder alisema : “Wilder kushinda ni vizuri kwa sababu (pambano lake dhidi yangu) ni kitu watu wanatamani kitokee.
“Lakini ninafiriki Fury anaweza kushinda. Kwa Wilder kushinda anatakiwa kumpiga Fury kabisa, na hakuweza kufanya hivyo mara ya kwanza.
“Fury ana vitu vingi katika ghala yake ya silaha ndio maana ninaegemea kwake.”
“Kila la kheri kwa Fury- itakuwa vizuri kuwa na mabingwa wawili wa uzito wa juu hapa England.”