KLOPP AWAPA ONYO ATLETICO
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewaonya Atletico Madrid kuwa mechi bado haijakwisha baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza katika dimba la Wanda Metropolitano.
Jurgen Klopp amepigwa goli 1-0 katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 bora Klabu bingwa Ulaya na mechi ya marudiano itapigwa Anfield baada ya wiki tatu.
“Kubakia katika mechi kama hii, kwetu sisi ni maendeleo,” Klopp alisema baada ya mechi.
“Tumekuwa na michezo katika mazingira kama haya ambapo tulipoteza umakini kidogo na kisha wangeweza kufunga goli la pili au vyovyote na hilo halikuonekana usiku wa leo”
“Sasa ni mapumziko, tupo nyuma 1-0. Tusingeweza kukata tamaa kama tuna dakika 15 za mapumziko, kwa nini tukate tamaa kama tunazo wiki tatu (za mapumziko)?”
Mashabiki wa Atletico Madrid walichangia ushindi wa timu yao hapo jana kwa kuishangalia tangu kabla ya mechi mpaka mwisho wa mchezo na kupelekea kocha wao Jurgen Klopp akawapa sifa baada ya mchezo
“Tulianza kushinda mechi tulivyofika Roundabout tukiwa njiani kwenda uwanjani.
“Mapokezi yalikuwa yakuvutia. Katika miaka nane nimekuwa klabuni, sijawahi kuona mapokezi kama hayo.” Alisema Simeone
Hata hivyo Klopp amewaonya Atletico Madrid kuhusu Anfield na anaamini mashabiki wao wataamua mchezo wao wa marudiano.
“Kipindi cha pili tutacheza katika uwanja tofauti, katika uwanja wetu, na hilo litakuwa tofauti pia.” Amesema Klopp
“Nimeona sura nyingi za furaha kwa Atletico usiku wa leo. Ni ushindi mkubwa, lakini mechi bado haijakwisha”
“Kwa vile tunaweza kuwa na wachezaji 11 wenye jezi ya Liverpool, tutajaribu kwa yote tuliyonayo.
“Kwa Mashibiki wa Atletico watakaopata tiketi ya mechi —karibuni Anfield”