TP MAZEMBE WASHINDWA KUWEKA KAMBI MOROCCO KWA SABABU YA SERIKALI
Timu ya TP Mazembe wamesitisha kambi yao waliyopanga kuweka nchini Morocco kuelekea mchezo wao wa robo fainali klabu bingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca Februari 28.
Imeelezwa kuwa Mazembe wamefanya maamuzi hayo baada ya serikali ya Congo kuvunja ahadi yao ya kuwafadhili katika siku watakazokuwepo Morocco.
TP Mazembe wamethibitisha kuahirishwa kwa kambi yao kupitia Meneja wao.
“Kupewa ahadi batili na huduma chaguzi na serikali ya Congo juu ya usimamizi wa TP mazembe, na kama ilivyopingwa na FECOFA (Chama cha soka cha Congo), uongozi haukuwa na chaguo ila ni kuahirisha kambi” aliandika katika Twita Meneja wa timu hiyo
Mabingwa hao wa zamani wa Afrika, sasa wanapeleka macho yao katika michuano yao ya ndani,wakiwa na mechi Jumapili ya wiki hii kabla ya kupaa kwenda Morocco Jumatatu—siku nne kabla ya mechi yao na Raja Casablanca ambao watarudiana wiki moja baadae mjini Kinshasa,Congo