MAN CITY WAJIBU KUHUSU KUFUNGIWA NA UEFA,WAAHIDI KUPINDUA MEZA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Manchester City Ferran Soriano amesema kuwa tuhuma za UEFA kuhusu timu yao si za kweli na watahakikisha wanathibitisha hilo kabla ya majira ya kiangazi mwaka huu na kifungo chao kuondolewa.
Ijumaa iliyopita, Manchester City ilitangazwa kufungiwa kushiriki michuano ya Ulaya kwa misimu miwili na UEFA kwa kosa la kuvunja sheria ya matumizi ya fedha “Financial Fair Play”.
Soriano ameyasema hayo leo katika mahojiano maalum na kitengo cha habari cha klabu yao
“Vizuri, kitu muhimu zaidi ninachopaswa kusema leo ni kuwa tuhuma ni za uongo. Si za ukweli.
“Mashabiki wanaweza kuwa na uhakika na vitu viwili. Kwanza ni kwamba tuhuma si za kweli . Na Pili ni kwamba tutafanya kila kitu kuthibitisha hilo.
Soriano amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa watafanya kila kitu ili kupita changamoto hii na kutowaangusha.
“Mmiliki wa klabu hajaweka pesa katika hii klabu ambazo zimekuwa hazijulikani. Sisi ni klabu endelevu, yenye faida, hatuna madeni, akaunti zetu zimekuwa zikichunguzwa mara nyingi na wakaguzi, na wasimamizi, na wawekezaji na hili lipo wazi kabisa” alisema Soriano
“Tunaangalia utatuzi wa mapema ni wazi kupitia njia ya uhakika na njia ya haki. Kwa hiyo matumaini yangu ni tutamaliza kabla ya kuanza kwa majira ya kiangazi.”
Baada ya kifungo hicho Manchester City wanataraji kwenda katika mahakama ya usuluhishi ya michezo (CAS) ili waweze kuondolewa kifungo hicho pale itakapothibitika hawana makosa.