TSHABLALA AKANA WACHEZAJI WA SIMBA KUMCHOMESHA KOCHA
Mohamed Hussein Tshabalala amekanusha taarifa zinazoenezwa kuwa Simba SC kutokupata matokeo mazuri na kutocheza vizuri kunatokana na wachezaji hao kuwa katika mgomo baridi dhidi ya kocha wao Sven Vanderbroeck.
Hivyo ni kama walikuwa wamegoma ili timu isifanye vizuri na kocha Sven afukuzwe, Mohamed Hussein amejibu kuwa sio kweli walitelez ndio maana katika mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar wamerekebisha makosa na kushinda 3-0, hivyo kutokufanya kwao vizuri yalikiwa makosa ya kawaida.
“Sio kweli unajua siku zote timu inapofanya vibaya kila aina ya maneno yatazungumzwa, kwa hiyo tumedhiirisha kuwa tuliteleza na leo tumenyayuka waendelee tu kutusapoti waachane na maneno maneno” alsema Mohamed Hussein
Simba SC katika mchezo dhidi ya Mtibwa uliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro walishinda kwa mabao 3-0, mabao yakitiwa wavuni na John Bocco dakika ya nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, Mohamed Hussein dakika ya 47 na Hassan Dilunga dakika ya 59.