Arsenal nusura wavunje rekodi yao
Kikosi cha Arsenal kilichochini ya kocha Mkuu Unai Emery kimenusurika na kipigo katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates, katika mchezo wa Ligi Uingereza dhidi ya Wolverhampton Wanders.
Arsenal wamenusurika na kipigo kutoka kwa Wolverhampton, baada ya goli la Henrikh Mkhitaryan dakika ya 86, ikiwa ni dakika chache baada ya kuingia akitokea benchi dakika ya 76, Mkhitaryan anainusuru Arsenal ikitoka nyuma kwa goli 1-0 lililofungwa na Ivan Cavaleiro wa Wolverhampton mapema kabisa dakika ya 13 ya mchezo lakini Mkhitaryan kaufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufunga bao 1-1.
Mchezo ulikuwa wa kuvutia kutoka na Arsenal kuendeleza na utamaduni wake wa kupenda kumiliki mpira na pasi, pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 71 kwa 29 dhidi ya Wolverhampton haikusaidia kupata ushindi zaidi ya kunusurika kuvunja rekodi yao chini ya Kocha Unai Emery.
Arsenal kama angekubali kupoteza mchezo leo angekuwa ana ruhusu kupoteza mchezo kwa mara ya kwanza chini ya kocha Unai Emery, akiwa kaiongoza katika mechi 16 za hivi karibuni za mashindano yote mfululizo pasipo kupoteza mchezo wowote, Unai Emery ndio kocha aliyemrithi Arsene Wenger.
Sare hiyo imewafanya Arsenal waendelee kubaki nafasi ya tano kwa kuwa na alama 24 tofauti ya alama tatu na Tottenham aliyepo nafasi ya nne kwa alama 27 wote wakicheza michezo 12 tayari ya Ligi Kuu, Wolverhampton wapo nafasi ya 11 wakiwa na alama 16 wakicheza michezo 12 kama ilivyo kwa Arsenal, hiyo ni baada ya kuhakikisha leo hawaruhusu kipigo cha tano Ligi Kuu.