WAZIRI ASEMA CORONA HAIWEZI KUZUIA MICHUANO YA OLIMPIKI JAPAN
Waziri wa Olympiki Japan, Seiko Hashimoto amesema hakuna mipango ya kughairisha michuano ya Olimpiki inayotaraji kufanyika nchini Japan kuanzia mwezi Julai mwaka huu kutokana na uwepo wa virusi vya Corona ambavyo vimesababisha vifo 361 nchini China mpaka sasa.
Mwanamama huyo,55, ambaye zamani alikuwa akicheza Speed Skating na mbio za baiskeli, amesisitiza kuwa waandazi hawana mpango wa kuaghirisha michuano hiyo ambayo inataraji kuanza Julai 24 na kumalizika Agosti 09.
Pia,waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amethibitisha serikali watakuwa karibu na makundi yote muhimu kuhakikisha virusi hivyo haviathiri kufanyika kwa michuano hiyo mwaka huu.
“Tutakuwa karibu na kila mtu, wakiwamo kamati ya kimataifa ya Olimpiki na Shirika la Afya Duniani, kuchukua hatua stahiki na kufanya virusi vya Corona haviathiri Olympiki” – Abe aliiambia kamati ya Bunge la Japan.