MASHABIKI WA SIMBA WAMLILIA AUSSEMS ‘UCHEBE’
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Mbelgiji Patrick Aussems, ameandika katika kurasa wake wa Instagram kuhusu kuguswa na mashabiki wa Simba kumkata arejee katika timu hiyo
“Nimeguswa sana na maelfu ya meseji nilizopokea katika siku chache zilizopita zikinitaka nirudi. Simba SC ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri na mashabiki wazuri. Ninawatakia kheri na nina hakika kuwa siku moja tutakutana tena.” – Ameandikwa kocha huyo
Kocha huyo anaandikwa hivyo ikiwa zimepita saa kadhaa tangu Simba ipoteze mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania na kupelekea mashabiki wa timu hiyo kutaka kocha wao wa zamani arudishwe.
Simba ilimfukuza Patrick Aussems Novemba 30 mwaka jana baada ya kudumu nae kwa muda wa zaida ya mwaka mmoja na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa sasa Sven Vanderbroeck kutoka Ubelgiji.