JULIO AKOMAA NA UMRI WA WACHEZAJI SIMBA
Kocha wa zamani na mchezaji wa zamani wa Simba SC Jamhuri Kiwelu “Julio” amefafanua kauli yake ya kusema wachezaji wa Simba SC wazee.
Julio akihojiwa na Kipenga Xtra ya East Africa Radio ameeleza kuwa kauli yake hiyo ina maanisha kuwa wachezaji hao umri umeenda na wamechoka kwa mikiki mikiki.
“Kwenye kweli nasema kweli, kuna watu wanasema nirudishe kadi ya Simba. Hivi wanajua kiasi gani sisi tumeipigania hii timu mpaka hapa. Kwanza mimi ni mtu ambaye hivi sasa ninaishi maisha mazuri kwa sababu ya Simba, ila nawaambia ukweli”
“Mimi ninaposema Simba ina wachezaji wazee, simaanishi kuwa kina Kagere au Bocco wana miaka 70, ila ninamaanisha kuwa wachezaji wetu wametumika sana hivyo hawaendani na mikiki mikiki ya vijana”