AZAM NA KMC WANYAKUA TUNZO ZA VPL
Mshambuliaji wa KMC Sadallah Lipangile ameshinda tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi Januari wa VPL akiwashinda Nicholas Wadada wa Azam FC na Hassan Dilunga wa Simba waliokuwepo katika kinyang’anyiro hicho
katika mwezi Januari, Sadallah Lipangile alifanikiwa kufunga magoli manne, magoli mawili akifunga katika ushindi wa 2-0 wa ugenini dhidi ya Singida United na mengine mawili katika ushindi wa nyumbani wa 2-0 dhidi Mtibwa Sugar.
Kocha wa Azam FC Aristica Cioaba amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Januari wa VPL baada ya kuwashinda kocha wa Simba SC Sven Vandenbroeck na Malale Hamsini wa Polisi Tanzania.
Hii ni tuzo nyingine anaiongeza kwenye kabati lake baada ya kushinda ile ya mwezi Novemba mwaka jana.