KIFO CHA KOBE CHAMKOSESHA AMANI KAWHI LEONARD KUSAFIRI NA HELICOPTER
Alipokuwa anarejea Los Angeles kuicheza Clippers, Kawhi Leonard alimtafuta rafiki na mshauri wake Kobe Bryant kwa ajili ya ushauri juu ya mambo mengi kuanzia mpira wa kikapu, sehemu ya kuishi mpaka namna ya kusafiri na kuzunguka hapa na pale Los Angeles.
Kawhi amesemsa Kobe ndiye mtu aliyemshawishi kutumia usafiri wa Helicopter na kwenda mbali zaidi kwamba sio tu kutumia usafiri huo bali hadi kumtumia rubani wake Ara Zobayan ambaye nae ni moja wa wahanga katika ajali hiyo. “Niliona namna akiwa anaetoka na kwenda Newport na akaniambia amekuwa akifanya hivyo kwa miaka 17 na kitu sasa.”
Kawhi mwenye makazi karibu na uwanja wa Staples Center anaishi nyumbani kwake San Diego alisema “Kuanzia rubani hadi kila kitu, utaratibu wote wa usafiri (helicopter) ninaotumia kuja na kutoka hapa (Staples Center) tokea San Diego.
Zobayan alikuwa mtu mazuri sana, rubani bora kabisa ambaye unaweza mwomba akutoe mji mmoja kwenda mwingine bila wasiwasi. Atanishusha mimi na kuniambia anaenda mchukua Kobe ama atakuja nichukua na kuniambia Kobe amenisalimia ama nimemshusha Kobe muda sio mrefu na mambo kama hayo.” Nyota huyu amesema bado hajaweza fikiria kama atasimama kwa muda tumia usafiri huo ama ataendelea nao baada ya ajali hiyo ya siku ya Jumapili.