SIMONA HALEP NA MUGURUZA WAFIKA NUSU FAINALI AUSTRALIAN OPEN
Mwanadada Simona Halep amefanikiwa ingia hatua ya nusu fainali ya Australian Open kwa kumtoa Mestonia Anett Kontaveit kwa seti 6-1 6-1 katika mechi ya dakika 53.
Halep hajapoteza seti yeyote hadi sasa huku akionyesha kuendeleza rekodi yake baada ya kuonekana kumzidi nguvu Kontaveit.
Matokeo haya yatamfanya kukutana na bingwa wa Grand Slam mara mbili Gabrine Muguruza, Muguruza akiwa ameshinda mechi dhidi ya Mrusi Anastasia Pavlyuchenkova kwa jumla ya seti 7-5 6-3.