KOBE BRYANT, BINTI YAKE NA FAMILIA YA ALTOBELLI WAPOTEZA UHAI KWA AJALI
Nguli wa mchezo wa basketball Kobe Bryant, 41, nab inti yake Gianna, 13, wamepoteza maisha katika ajali ya iliyohusisha takribani watu tisa wao wakiwa miongoni mwao.
Braynt alikuwa akielekea katika kituo cha mpira wa kikapu na binti yake Gianna mapema Jumapili asubuhi kabla ya helicopter waliyokuwa wamepanda kuanguka na kulipuka.
Kiongozi wa usalama wa jiji la Los Angeles Sherrif Alex Villanueva alisema hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo ambayo kulingana na manifest ya abiria inaonyesha kuwelikuwepo na awatu 9 katika helicopter hiyo tofauti na taarifa za watu 5 hapo awali.
Mamlaka ya zimamoto ya jiji hilo imesema mamalaka ya anga ipo eneo la tukio na watashughulika na mamlaka ya taifa ya usalama na usafirishaji kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiongeza kuwa hawatatoa majina ya wahanga mpaka pale watakapotambulika na watu wa karibu kupatiwa taarifa.
Chanzo cha ajali bado hakijajulikana hadi hapo uchunguzi utakapokamilika. Helicopter hiyo iliondoka katika uwanja wa John Wayne Airport majira ya saa 3:06 asubuhi (saa za Marekani) na taarifa ya kwanza juu ya ajali kutolewa saa 3:47.
Familia ya Altobelli imedhibitisha kuwa, kocha wa timu ya kikapu ya chuo cha Orange Coast gwiji John Altobelli, mkewe (Bi. Keri Altobelli), na mtoto wao Alyssa Altobelli ni miongoni mwa wahanga katika ajali hiyo.
Ajali hii imetokea siku moja baada ya Kobe Bryant kupitwa na LeBron James katika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote NBA na Kobe kuwa moja ya watu waliompongeza LeBron kwa hatua hiyo huku akifanya hivyo saa 4 usiku wa Jumamosi.
Kobe aliyecheza NBA kwa miaka 20 alistaafu mwezi APRIL 2016 akishinda tunzo za MVP 2008, ubingwa wa Olimpiki mara 2 na tunzo nyingine nyingi ikiwa ni pamoja na ya Oscar ya filamu fupi bora yam waka kutokana na filamu yake ya dakika 5 ya Dear Basketball inayoelezea mapenzi yake kwa mchezo huo.
Kobe na mkewe Vanessa walifanikiwa kuwa na familia ya watoto wanne wa kike Natalia, Bianca, Capri na Gianna.