KABWILI WA YANGA AFUNGUKA HONGO YA IST KUTOKA SIMBA
Mlinda mlango wa Yanga SC Ramadhani Kabwili leo alikuwa katika mahojiano maalum na East Afrika Radio na ameeleza kuwa aliwahi kushawishia na watu wa Simba iliajipatishe kadi ya njano makusudi ili aukose mchezo dhidi ya Simba.
“Simba waliwahi kunifuata kipindi tupo na kocha Zahera, nilikuwa na kadi 2 za njano na kwenye mchezo wa Yanga na JKT Tanzania, walitaka nitafute kadi ya njano makusudi ili wanipe gari ya IST mpya na nikose mchezo ujao wa watani” – Ramadhan Kabwili
Kabla ya mchezo wa watani wa kadi Simba na Yanga Kabwili alikuwa tayari ana kadi ya njano hivyo kuelekea mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania kama angeoneshwa kadi ya njano nyingine asingeweza kucheza mchezo unaofuatia kutokana na kuwa na kadi tatu za njano ambazo kikanuni anakosa mechi moja.