REAL MADRID WATOA HESIMA KIFO CHA KOBE BRYANT
Wachezaji wa Real Madrid chini ya kocha wao Zinedine Zidane leo kabla ya kuanza mazoezi ya timu hiyo walisimama kimya kwa dakika moja (moment of silence) kutoa heshima zao kwa ajili ya kifo cha mchezaji Basket Kobe Bryant.
Kwenye mazoezi hayo kabla ya kuanza Sergio Ramos alionekana kuingia mazoezini akiwa na jezi ya timu ya taifa ya kikapu ya Marekani namba 10 ikiwa na jina la Kobe Bryant kama ishara ya kumuenzi staa huyo wa NBA.
Bryant ,41, ambaye ni nyota wa zamani wa Los Angeles Lakers na NBA alipata ajali ya helikopta jana na kupoteza maisha jumla ya watu tisa akiwemo yeye na binti yake Gianna Maria-Onore ,13,.