ANTONY JOSHUA ATAFUTA PAMBANO JIJIN KINSHASA NCHINI CONGO
Promota Eddie Hearn amethibitisha kuwa na vikao vitakavyopelekea bondia Antony Joshua kupigana pambano katika uwanja maarufu uliohodhi pambano la nguli Mohamed Ali jijini Kinshasa nchini Congo miaka ya nyuma
katika pambano lililopewa jina la ‘Rumble in the Jungle’ na bondia Muhammad Ali alimpiga kwa Knock Out George Foreman na kufanikiwa shinda ubingwa wa dunia wa uzani wa juu mwaka 1974.
“Ni moja kati ya viwanja maarufu sana vya ngumi vya muda wote, DRC wanaangaza namna ya kurudisha uwanja huo katika hadhi, jambo ambalo ni zuri”

“Kumekuwa na vikao vilivyofanyka juu ya swala hili lililoletwa kwetu nan i jambo ambalo tutaliangalia. Joshua anataka kuweka historia, ukiangalia katka wasifu wake amepigana kila mahali, UK, Madison Square Garden na Saudi Arabia, kuiweka Africa, China na Mashariki y Mbali katika wasifu hapo ndipo unapata tambulika kuwa na hadhi kidunia.” Alisema Hearn alipokuwa kaihojiwa katika kipindi cha 5 Live Boxing.
Joshua alirejesha mikanda yake ya ubingwa toka kwa Andy Ruiz Jr mwezi Desemba 2019 nchini Saudi Arabia baada ya ushindi wa point.
Joshua anatarajia kupigana nchini Uingezeza kwa sasa baada ya kupigana nje ya hapa kwa muda huku Mbulgaria Kubrat Pulev akiwa ndiye mpinzani anayetazamiwa zaidi kupewa nafasi ya kupanda nae ulingoni.
Viwanja vya klabu za Arsenal, Totteham na Westham ni viwanja vinavyopendekezwa zaidi kwa ajili ya pambano la Joshua linalofata hususani akihusishwa kucheza dhidi ya Pulev.