MASHABIKI WAVAMIA NYUMBA YA ED WOODWARD
Nyumba ya makamu mwenyekiti wa klabu ya Manchester United Ed Woodward imevamiwa na kundi la watu waliokuwa wakiimbia nyimbo za ghadhabu huku video moja iliyorushwa mtandaoni ikionyesha mmoja wao akirusha baruti juu ndani ya makazi ya hayo.
Woodward, 48, mwenye familia ya mke na watoto wawili, hakuwepo muda wa tukio hilo. Klabu ya Manchester imetoa tamko ikisema yeyote anayefanya kosa la jinai namna hiyo atafungiwa maisha na pia kuwa ni haki kwa mashabiki kuonyesha hisia zao ila sio kwa ktishia maisha ya mtu mwingine.
Woodward aliyekuwa mshari wa Malcom Glazer na familia ya Glazer katika ununuzi wa klabu hii mwaka 2005, amekuwa akipokea upinzani mkali toka kwa mashabiki kutokana na matokeo mabaya ya uwanjani ya timu hiyo.