COCO GAUFF AMTUPA NJE BINGWA MTETEZI NAOMI OSAKA
Siku ya leo haionekani kuwa siku nzuri kwa nyota wa tennis upande wa wanawake na ikiwa ya bahati kwa chipukizi. Kinda Coco Gauff amefanikiwa kumtoa bingwa mtetezi Naomi Osaka akimfunga kwa jumla ya seti seti 6-3 6-4.
Akiongea baada ya mechi Gauff alisema “Miaka miwili iliyopita nilipoteza katika raundi ya kwanza kwenye mashindano ya watoto na sasa nipo hapa. Leo nilikuwa najiambia tu mara kadhaa, pambana hujuui ni nini kinaweza tokea”
Gauff sasa atakutana na Mchina Zhang Shaui ama Mmarekani Sofia Kenin katika raundi ya nne.

Akiongea baada ya kipigo Osaka alisema “Bado sina ari ya ubingwa kwamba naweza shinda nikiwa katika hali ngumu mchezoni. Kuna muda nazidiwa na sijui nifanye nini.
Pia nina tatizo la umri. Sipendi kufungwa na mtu mwenye umri mdogo kuliko mimi na hili nimelichukulia kwa ubiafsi zaidi.”