DJOKOVIC ASONGA MBELE ASUTRALIAN OPEN
Bingwa mtetezi Novack Djokovic ametinga hatua ya raundi ya nne baada ya kumtoa Yoshihito Nishioka kwa seti 6-3 6-2 6-2. Djokovic alikuwa na mchezo mzuri na wa ari akipoteza ‘serve’ moja two katika seti mbili za mwanzo akishinda asilimia 93 ya pointi zake katika serve ya kwanza.
Djokovick sasa atakutana na Diego Schwartzman aliyefanikiwa kumtoa Dustan Lajovic wa Argentina kwa seti 6-2 6-3 7-6 (9-7). Akiongelea juu ya kukutana na Schwartzman, Djokovic amesema “Kama nitakuwa na ‘serve’ nzuri kama za leo basi nitakuwa na nafsi ya kushinda. Schwartzman ni mchezaji mzuri katika ATP”