MCHINA AMTUPA NJE SERENA WILLIAMS AUSTRALIAN OPEN
Serena Williams ametolewa katika mashindano ya Australian Open na Mchina Wang Qiang anayeshika nadfasi ya 27 kwa ubora akifungwa kwa jumla ya seti 6-4 6-7 (2-7) 7-5, hii ikiwa ni mapema zaidi kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2006 alipotolewa na Daniela Hantuchova. Akiwa haamini katika kile kilichotokea nyota huyo aliyefanya makosa mengi alisema “Siwezi cheza hivi, siwezi tena. Hii sio sawa. Kusema kweli sikutegemea poteza mchezo huu. Kwa matokeo haya kesho naanza mazoezi.”
Bingwa huyu wa Australian Open mara 7 na Grand Slam 23 anaendelea weweseka katika kutafuta fikia rekodi ya mwanamke mwenye Grand Slam nyingi inayoshikiliwa na Margaret Court mambo yakiwa yanamwendea kombo kuanzia fainali ya US Open 2008 alipofungwa na Mjapani Naomi Osaka.