BARCELONA KWENDA VISIWA VYA RAHA VYA IBIZA
Kikijulikana kama kisiwa cha mapumziko, watu mashuhuri na klabu za usiku, klabu ya Barcelona itakuwa katika kisiwa hiki Jumatano hii.
Tofauti na mapumziko, muziki na kufurahia maisha, Barcelona watakuwa kisiwan hapo kwa ajili ya kucheza mechi yao ya mzunguko wa 32 katika kombe la Copa del Rey dhidi ya klabu ya UD Ibiza.
Hii ni mara ya kwanza kwa kisiwa hiki kupata ugeni wa timu kubwa kucheza dhidi ya timu yao iliyopo Segunda Division B ikitafuta nafasi ya kushiriki ligi daraja la pili. Mauzo ya tiketi za mechi hii yameongezeka toka watu 4,500 mpaka watu 6,445 kutokana na ukubwa wa mechi hii.
Kabu hii imemchukua Dj maarufu Manu Gonzalez kupiga mziki kipindi cha mapumziko na kusherehesha mechi hiyo. Timu hii iliyoundwa mwaka 2015 kuchukua nafasi ya UD Ibiza-Eivissa ilishawahi weka logo ya klabu ya usiku kwenye nafasi ya logo ya timu jambo amabalo lilikemewa vikali na kingozi anayewapa sapoti kwa kusema “Wao sio klab ya usiku nan i kukosa nidhamu kwa kitendo kama hicho.”