IFAHAMU TIMU YA WANANCHI ILIYOCHEZA NA REAL MADRID
Klabu ya Real Madrid imefanikiwa ingia hatua ya 16 bora katika michuano ya Copa Del Rey baada ushindi wa goli 3 – 1 dhidi ya Unionistas de Salamanca.
Unionistas ni klabu inayomilikiwa na mashabiki wa soka takribani 2,800 ambao wote hulipa ada na wote wana nguvu sawa katika klabu hiyo yani demokrasia. Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa manispaa na ni wanachama 50 waliweza wahi mapema na kufanya maandalizi ya uwanja huo kwa ajili ya mechi baada ya kukataa kucheza katika uwanja mkubwa wanaoutumia wapinzani wao.
Mmoja ya waandamizi wa klabu hiyo akizungumza na John Bennett wa BBC aliweza tuma picha wakiwa wanafanya maandalizi.
Mashabiki waliunda klabu hii mwaka 2012 baada ya klabu UD Salamanca kushindwa jiendesha kibiashara.
Walidhamiria fanya kazi kwa pamoja na kutorudia makosa hayo. Maamuzi yote katika klabu hadi muonekao wa jezi na vifaa vya klabu hupita kwa kupigiwa kura huku shughuli zote zikifanywa na watu wanaojitolea ikiwamo wakurugenzi wa klabu.
Wanasimamia misingi na tamaduni zao ikiwa ni pamoja na kutopokea matangazo toka kampuni za kubashiri (betting) pamoja na mitandao ya ponografia huku wakiwa wamejiwekea dhumuni la pamoja la kutenga kiasi cha faida kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii.