LUC EYMAEL AONJA USHINDI WAKE WA KWANZA YANGA
Klabu ya Yanga SC ikiwa chini ya kocha wake Luc Eymael leo imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza chini ya kocha huyo wakiwa Singida.
Wakiwa wageni wa Singida United leo Yanga wamepata alama tatu muhimu kufuatia ushindi wa magoli 3-1 waliyoyapata na hatimae Luc Eymael kuonja utamu wa ushindi kwa mara ya kwanza.
David Molinga ndio ameendelea kuwa mfungaji wa Yanga akifunga bao la kwanza dakika ya 12, Haruna Niyonzima dakika ya 58 kabla ya mshambuliaji wao raia wa Ivory Coast Yikpe kufunga goli la mwisho dakika ya 77 na kuwa goli lake la kwanza toka awasili Tanzania.