BADO NIPO CITY, LABDA WANIFUKUZE – GUARDIOLA
Baada ya kufanikiwa kushinda ubingwa wa EPL misimu miwili mfululizo huku msimu huu wakioneka kuelekea maliza katika nafasi ya pili chini ya vinara Liverpool wanaoongoza ligi kwa tofauti ya point 14, bosi huyo wa Manchester City amedai kuwa ataendelea baki klabuni hapo msimu ujao labda kama wakimfukuza. Hii ni baada ya uvumi kuwa kocha huyu anaweza akatumia kifungu kinachomwezesha kuvunja mkataba wake unaoisha mwaka 2021.
Akiongea jana kabla ya mechi yao na Crytal Palace alisema “Sisemi nabaki sababu tumeshinda michezo yetu miwili ya mwisho. Hata kama tungekuwa tumefanya vibaya siendi popote.”
“Labda wanifukuze, ila nipo hapa kwa asilimia 100” alisema Guardiola ambaye timu yake ilifanikiwa shinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Manchester United na ule wa ligi dhidi ya Aston Villa kwa magoli 6 – 1.
“Hakuna kocha anayeshinda kila mechi. Tumepoteza michezo michache, ni kurudi na kuweka juhudi tufanye vizuri.”
Guardiola alijiunga na City mwaka 2016 ambapo amefanikiwa kuchukua ubingwa waligi kwa rekodi ya kufikisha pointi 100 huku akiwa ni kocha wa kwanza kuchukua mataji yote matatu ya mashindano ya ndani (EPL, FA na Carabao) England.