SUAREZ ATAJA GOLI LAKE
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez amelitaja goli lake alilofunga dhidi ya Mallorca juzi jumamosi ndio goli lake bora kuwahi kufunga katika maisha yake ya soka.
Suarez alifunga goli hilo Barcelona wakiondoka na ushindi wa goli 5-2, huku bingwa mara sita wa Ballon d’Or Lionel Messi akiweka rekodi ya kufunga hat trick 35 katika LaLiga, na kuwa mchezaji aliyefunga hat trick nyingi kuliko mwingine yoyote. Cristiano Ronaldo anashika nafasi ya pili akifunga hat trick 34.
“Ni goli bora katika maisha yangu.
Nilijua kuwa ilikuwa ni pembe ngumu na chaguo la mwisho nililokuwa nalo ilikuwa kupiga kwa kisigino changu.” Alisema Luis Suarez baada ya mchezo huo.
“(Kocha mkuu) Valverde ananiambia kwamba muda mwingine huwa ninakosa magoli rahisi na kufunga magoli magumu “
Ushindi huo uliirudisha Barcelona kileleni na kuishusha Real Madrid kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, huku wakiwa wamelingana pointi.