NI VIGUMU KUPATA MBADALA WA MESSI BARCELONA
Rais wa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania Josep Maria Bartomeu amekiri kuwa haoni nani anaweza kuja kuwa mbadala wa Lionel Messi Camp Nou kutokana na nyota huyo kufanya mambo makubwa klabuni hapo.
Josep Maria Bartomeu amekiri kuwa atampa ofa ya kusaini mkataba wa maisha mchezaji huyo kwani hana mbadala.
Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache zimepita toka Messi awe mchezaji pekee aliyeshinda tuzo ya Ballon d’Or mara 6.
Bartomeu anaamini kuwa kupata mbadala wake ni ngumu lakini wameamua kuanza kwa kuongeza uwekezaji kwa soka la vijana ambapo ndio alipoibuliwa Lionel Messi.
“Leo ni hawezekani kupata mbadala wake na kipindi atakachokuwa hayupo hapa tena , itatulazimu kucheza tofauti . Siwezi kusema tayari tumejiandaa na maisha baada ya Messi, lakini ni kweli kwamba tayari tumeamua kuweka dau kwa wachezaji wadogo kwa muda mrefu” aliongea Rais huyo akihojiwa na gazeti
la Italia la La Repubblica
Bartomeu pia ameweka wazi kuwa suala la Pep Guardiola kurudi Nou Camp lipo mikononi mwa Guardiola mwenyewe ambaye aliondoka 2012 na kujiunga na FC Bayern na sasa Man City baada ya kushinda mataji manne ndani ya msimu mmoja.
“Uwezekano wa Pep Guardiola kurudi? hilo halitegemeani na mimi, Pep mwenyewe ndio aliamua kuondoka lakini kwa upande wake milango ya yeye kurejea hapa (Barcelona) siku zote ipo wazi”