VAR YAANZA TUMIKA AFRIKA
VAR ikileta mkanganyiko na kuendelea kukataliwa katika ligi kuu nchini England, nchini Morocco imeandikwa historia mpya, kwa nchi hiyo kuwa ya kwanza kutumia teknolojia hiyo kwa mashindano ya ndani barani Afrika.
Ni katika nusu fainali za michuano ya ndani nchini Morocco hapo jana ndio teknolojia hiyo ilianza kutumika, TAS Casablanca wakicheza dhidi ya Difaa El Jadida anayoichezea winga wa kimataifa wa Tanzania Saimon Msuva.
Katika dakika 120 na VAR ilitumika kufanya maamuzi yaliyoipatia penati Casablanca na kuipa ushindi wa goli 1 – 0 katika mchezo huo.

Nusu fainali nyingine itakuwa ni kati ya Hassania Agadir dhidi Maghreb Atletico Tetwan leo Jumapili jijini Marrakech nayo itakuwa na VAR.
VAR ilitumika katika michuano ya AFCON 2019 nchini Misri kuanzia hatua ya robo fainali.