JAMES HARDEN AENDELEZA UBABE NBA
Katika mechi za usiku wa kuamkia leo za NBA, mchezaji James Harden ameshindwa kuandika ‘Triple double’ yake ya kwanza msimu huu akifunga points 42, rebounds 10 na assists 9 wakati Rockets wakiondoka na ushindi wa pointi 117 – 94 dhidi ya Chicago Bulls ugenini. Mchezaji Russell Westbrook akiifungia Rockets points 26, rebounds 7 na assists 2.
Mechi nyingine ilikuwa kati ya GSW dhidi ya OKC, mechi iliyomalizika kwa OKC wakiwa nyumbani kuibuka na ushindi wa pointi 114 – 108 hii ikiwa ni mechi ya pili kwa OKC kiufunga GSW msimu huu.

Boston Celtics wamefankiwa kupata ushindi wa pointi 135 – 115 dhidi ya San Antonio Spurs huku Gordon Hayward akishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia mkono. Kemba Walker na Jaylen Brown aliyetupia pointi 30 waliiongoza vyema timu yao kupata ushindi.

Mechi nyingine ni Pelicans dhidi ya Hornets, Pelicans wakifanikiwa kubadili matokeo robo ya mwisho ya mchezo na kuondoka na ushindi wa pointi 115 – 110.
Dallas Mavericks wao walifanikiwa ondoka na ushindi wa pointi 138 – 122 dhidi ya Memphis Grizzlies Luka Doncic akikosa assist 2 kuandikisha ‘tripple’ double baada ya kufunga pointi 24, rebounds 14 na assist 8.