Kiungo wa Everton Andre Gomes, 26, aliyeumia vibaya Jumapili katika mechi dhidi ya Tottenham anatarajiwa rejea dimbani msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Gomes aliumia alipokuwa akikabwa na Son Heung-min na Serge Aurier, hali iliyopelekea kwa Son kuonyeshwa kadi nyekundu ambayo ilikuja kufutwa baada ya timu yake kukata rufaa.

Akiongea na waandishi wa habari kocha wa klabu hiyo Marco Silva alisema “Kila kitu kilienda sawa na tunatumaini tutamuona akicheza tena msimu huu. Hatuwezi kusema ni siku gani hasa atarejea ila kwa akili zetu na majibu tuliyopatiwa na jopo la madaktari ni kuwa inawezekana.”
Alipoulizwa kama Son ameongea na Gomes alisema “Hakika, na ulikuwa wakati mgumu kwa Andre ila hata kwa wengine wawili waliohusika Son na Aurier. Ukiangalia kwa makini ilikuwa ni ‘tackle’ ya nguvu. Nilikuwa wa kwanza kuangalia na ni wazi Son hakuwa na nia mbaya ila uwanjani uamuzi ni wa refa.”

Son Heung-Min hajashangilia magoli yake mawili ya kwanza tangu tukio hilo litokee, alifunga magoli hayo dhidi ya Red Star Belgrade katika klabu bingwa Ulaya juzi Jumatano, hakushangilia badala yake aliweka mikono yake kwa ishara ya kuomba msamaha kwa Andre Silva