KYLE WALKER AIDAKIA MAN CITY
Katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Atalanta na Man City usiku wa Novemba 06, dakika ya 46 kipa wa Man City Ederson alifanyiwa mabadiliko baada ya kuumia na nafasi kuchukuliwa na kipa Claudio Bravo.
Kunako dakika ya 81 Claudio Bravo akapewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Atalanta Josip Ilicic akiwa mtu wa mwisho.

Kocha wa Man City Pep Guardiola akiwa hana kipa mwingine katika benchi lake, ikabidi amtoe Riyad Mahrez na kumuingiza beki Kyle Walker akaenda kukaa golini mechi ikiwa 1-1.
Kyle Walker akafanikiwa kulinda goli na mechi ikaisha kwa sare ya 1-1.