Crouch katoa waraka kwa wanaoponda kuitwa kwa Rooney Uingereza
Kupewa heshima kwa nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney kucheza mchezo wa mwisho wa kimataifa wa Uingereza dhidi ya Marekani kumepokelewa vizuri na wanafamilia ya soka hususani kwa wachezaji soka wa Uingereza ambao wana majina.
Mshambuliaji wa Stoke City aliyewahi kucheza Liverpool Peter Crouch ni miongoni mwa wanasoka waliopokea wazo la Rooney kurudi kucheza mchezo wa mwisho wa Uingereza kwa furaha na amefikia hatua ya kukiri kuwa jambo hilo halijamshangaza na wala hatoshangaa akisikia Rooney kafunga katika mchezo huo.
Pamoja na hayo yote na wachezaji kusapoti kuitwa kwa Wayne Rooney lakini wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiikosoa FA kwa maamuzi waliofanya ya kumuita Rooney katika kikosi, Peter Croucha ameeleza kusikitishwa na wakosoaji wa jambo hilo.
“Tatizo ni nini? Nimekuwa nikisikia ukusoaji unaoilenga FA na Wayne kwa wiki yote hii na sijaelewa kabisa, hoja hiko hivi Rooney ameitwa katika kikosi cha Uingereza kucheza kwa mara ya mwisho lakini nimekuwa nikisikia wiki yote hii watu wakikosoa kuwa ni wazo baya wakati Rooney anarudi kama Surprise”alisema Crouch
“Najua baadhi yenu mtasema najaribu kumtetea Rooney katika hili kwa sababu ni rafiki yangu wa zamani lakini hoja ya msingi ni kwamba namjua Rooney (uwezo wake) na nilikuwa nikicheza nae pamoja katika kikosi cha Uingereza hakuna kingine kilichofanya niingie katika mjadala huu” alisema Crouch
Wayne Rooney atakuwa sehemu ya kikosi cha Uingereza kitakachocheza dhidi ya Marekani Alhamisi ijayo usiku licha ya kuitwa kwake kuwa na maneno maneno lakini Rooney ndio mfungaji bora wa Uingereza wa muda wote akiwa kafunga jumla ya magoli 53 katika mechi 119 katika miaka 13 akiichezea Uingereza na wiki ijayo atakuwa na fursa ya kuongeza mengine kama atafunga.