RONALDO KUNUNUA TIMU NYINGINE ULAYA
Ronaldo anataka kununua timu ya pili ya soka baada ya kuinunua Valladolid mwaka janaMshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldo Nazario amefichua kuwa anataka kununua timu pili ya mpira wa miguu baada ya mwaka jana kufanikiwa kuinunua Real Valladolid ya nchini Hispania mwaka jana.
Biashara ya kumiliki timu inaonekana kwenda vizuri kwa Mbrazil huyo na kumiliki timu moja ameona haitoshi na sasa anataka kuongeza timu nyingine.
Ronaldo alinunua hisa ya asilimia 51 za klabu ya Real Valladolid mwezi Septemba 2018, na sasa anataka kununua timu nyingine huko nchini Ureno.
Akizungumza katika mkutano wa mwaka wa teknolojia unaoitwa Web Summit ukifanyika Lisbon,Ureno Ronaldo amekaririwa akisema : “ Nilikuwa ninatafuta kununua klabu. Nilikuwa tayari nimeshaangalia England, katika daraja la pili. Ya kwanza ilikuwa ghali sana, na hata ya pili ilikuwa ghali pia.”
“Na pia nilitafuta Ureno, na bado ninatafuta ndani ya Ureno”
Katika msimu wa kwanza akiwa mmiliki wa klabu ya Real Valladolid, timu hiyo ilimaliza La Liga ikiwa nafasi ya 16 na sasa inashika nafasi ya 12.