SIMBA YAAMBULIA SARE KWA PRISONS
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara imeendelea leo uwanja wa Uhuru kwa Bingwa mtetezi Simba SC kucheza dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya.
Simba SC leo walikutana na kigingi cha Tanzania Prisons ambao tayari walikuwa wamecheza mechi 9 kabla ya mchezo wa leo wakiwa wameshinda mechi 3, sare sita na mchezo wa leo uliomalizika kwa sare 0-0 unakuwa ni mchezo wao wa 7 katika VPL msimu huu wanaondoka na sare.

Tanzania Prisons baada ya sare hiyo sasa wanakuwa nafasi ya 4 kwa kuwa na alama 16 na inabakia ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Kwa upande wa Simba SC ambao leo ni mchezo wao wa tisa wa VPL, hiyo ndio inakuwa sare yao ya kwanza msimu huu katika ligi hiyo baada ya ushindi wa mechi 7 na kupoteza mchezo mmoja.
Pamoja na kutoka sare hiyo Simba anaendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 22 akifuatiwa na Lipuli FC wenye alama 18 ila wameizidi Kagera Sugar kwa mchezo mmoja, Kagera Sugar wakiwa nafasi ya tatu na alama 17.