Hiki ndio kipindi kigumu kwenye maisha ya David Silva
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola aliwakusanya wachezaji wake katika chumba chao cha kubadilshia nguo cha timu hiyo katika uwanja wao wa Etihad mwezi December mwaka 2017 na kuwapa maagizo wanatakiwa washinde kwa ajili ya mchezaji mwenzao David Silva ambaye mtoto wake alikuwa amelazwa.
“Leo tunatakiwa tushinde kwa sababu moja , tushinde kwa ajili ya David Silva na mpenzi wake Yessica anahangahika kwa sasa katika maisha yake, sasa inabidi tushinde ili tukitoka pale tunafurahi kwa ajili yake na kama tukitoka pale tuwe tunaumia kwa ajili yake najua mnajua hali anayaopitia” alisema Pep Guardiola mwezi Desemba mwaka jana kabla ya mchezo wa Manchester City nyumbani dhidi ya Tottenham Hotspurs.
David Silva amekiri kuwa huo ndio ulikuwa wakati mgumu kwenye maisha yake aliowahi kupitia na ndio uliomfanya aachane na soka la kimataifa mapema mwaka huu kufuatia kuwa bize na matatizo ya kiafya ya mwanae Mateo ambaye alizaliwa akiwa njiti wa miezi mitano.
Hivyo ilikuwa inampa wakati mgumu kufikiria afya ya mtoto wake lakini pia kusafiri umbalu wa kutoka Manchester Uingereza hadi Valencia Hispania katika hospital ya Casa de Salud aliyokuwa amelazwa Mateo na mama yake, Silva akiwa hosptali Valenci alikuwa akifuatilia ushindi wa Manchester City 4-1 dhidi ya Tottenham na alifarijika kuona walifanya hivyo kwa ajili yake.
Mtoto wa David Silva anayejulikana kwa jina la Mateo pamoja na changamoto za kuzaliwa njiti wa miezi mitano, afya yake kwa sasa imeimarika yupo sawa na mwezi Agosti mwaka huu alimuonesha hadharani kwa mashabiki wa Manchester United waliokuwa wamejitokeza kwenye uwanja wa Etihad.