ARSENAL NA MAN UNITED ZAENDELEA FANYA VIBAYA EPL
Ligi kuu ya England imeendelea weekend hii huku mbio kati ya Liverpool na Man City zikionekana kutokupoa baada ya timu zote mbili kujinasua toka kwenye kipigo na kuchukua pointi zote 3 dakika za mwisho.
Manchester City dhidi ya Southampton walitoka nyuma dakika ya 70 kwa goli la Sergio Aguero na lile la Kyle Walker dakika ya 85 na kumaliza kwa goli ushindi wa goli 2 – 1 ,goli la Southampton likifungwa na James Ward dakika ya 13.
Liverpool wakiwa ugenini kwa Aston Villa walionekana kuambulia kichapo chao cha kwanza katika ligi msimu huu kwa goli la Trezeguet dakika ya 21 lakini dakika ya 87 Andy Robertson alibadili ubao kwa kusawazisha matokeo kabla ya Sadio Mane kufunga goli la ushindi ndani ya dakika 4 za nyongeza. Ilikuwa ni mechi iliyoshirikisha maamuzi ya VAR baada ya goli la Robert Firmino kukataliwa kipindi cha kwanza kwa sababu alikuwa ameotea.

Baada ya kulazimishwa sare dhidi ya Crystal Palace wiki iliyopita, timu ya Arsenal chini ya kocha Unai Emery leo imelazimishwa sare nyingine ya goli 1 – 1 na Wolves. Goli la Aubameyang dakika ya 21 halikitosha kuwapa ushindi baada ya Jimenez kuisawazishia Wolves dakika ya 76.
Manchester United chini ya Ole wakiwa ugenini kwa Bournemouth waliendelea kuweka rekodi kwa kushindwa kutunza clean-sheet katika mechi 11 za mwisho ugenini zikiwa ni nyingi tokea wafanye hivi msimu wa mwaka 2002/03.
Mechi hii iliisha kwa Bournemouth kuibuka na ushindi wa goli 1 – 0, lililowekwa kimyani na mchezaji wao wa zamani wa Man United Joshua King dakika ya 45.
Chelsea wakiwa ugenini dhidi ya Watford wameibuka na ushindi wa goli 2 – 1 magoli ya Chelsea yakifungwa na Tammy Abraham dakika ya 5 na Pulisic dakika ya 55 huku lile la Watford likifungwa dakika ya 80 na Gerard Deulofeu kupitia mkwaju wa penati.
Frank Lampard amekuwa ni kocha wa pili katika historia ya Chelsea kushinda mechi 7 za ugenini mfululizo katika michuano yote. Wa kwanza ni Bobby Campbell (Feb-April 1989)
Mechi nyingine zitaendelea kesho kwa Everton kuwakaribisha Tottenham huku Crystal Palace wakiikaribisha nyumbani Leicester City.