“ROMELU LUKAKU” AZIDI KUNG’ARA
Jiwe walilolikataa waashi ndilo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Ndivyo tunavyoweza kuelezea juu ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku.
Lukaku ameendelea kung’aa katika klabu yake mpya ya Inter Milan baada ya kufunga goli mbili, dakika ya 79 goli la kusawazisha na goli la ushindi dakika ya 90+1 , Inter inaondoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Bologna, goli la Bologna likifungwa na Roberto Soriano dakika ya 59.

Katika mechi nyingine Juventus wakiwa ugenini dhidi ya Torino wameibuka na ushindi wa goli 1 – 0 goli lililofungwa na De Light dakika ya 70.
Mbelgiji huyo sasa ana goli 9 za katika Serie A msimu akiwa nyuma ya Ciro Immobile wa Lazio mwenye goli 12.
Ushindi huu unawafanya Inter kubaki nafasi ya pili na pointi 28 nyuma ya vinara wa ligi Juventus wenye pointi 29 walizofikisha baada ya kushinda Turin Derby dhidi ya Torino.