AFRIKA KUSINI MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA RUGBY
Springboks wameibuka mabingwa wa Rugby Kombe la Dunia baada ya kuwafunga England 32-12 katika mechi kali na ya ushindani iliyojumuisha maamuzi ya TMO (Television Match Official) maarufu kama VAR katika mpira wa miguu.

Timu ya Afrika Kusini ilionesha kuwa bora wakiizidi England iliyokosa penati huku ikifanya makosa yaliyopelekea kufungwa kwa penati kuanzia dakika za mwanzoni.
Ukuta wa Afrika Kusini ulikuwa imara na kuwapa England ya kufunga ‘tries’ ama kupata penati mara kwa mara huku wachezaji Makazole Mapipi na Handre Pollard walikuwa katika viwango bora vilivyoisaidia Afrika Kusini pata ushindi mzuri wa mapema.

Ilikuwa fainali muhimu sana kwa Afrika Kusini iliyokuwa ikiongozwa na Siya Kolisi kapteni wa kwanza mweusi kuongoza kikosi hiki. Kolisi alizaliwa mwaka mmoja baada ya kumalizwa kwa ubaguzi wa rangi.
Afrika Kusini inaungana na New Zealand kuwa timu zinazoongoza kuchukua ubingwa wa Dunia, kila mmoja amechukua mara tatu.

Rais Jacob Zuma ndiye Rais pekee wa Afrika Kusini ambaye kipindi cha utawala wake timu ya Taifa haikushinda kombe la Dunia, Nelson Mandela walishinda mwaka 1995, Thabo Mbeki 2007 na sasa Cyrill Ramaphosa
Mchezo wa rugby ni moja ya mchezo mkubwa Afrika Kusini unaounganisha taifa hilo lenye watu wengi wenye tamaduni tofauti na lenye lugha rasmi zaidi ya 10.