MESSI APIGA GOLI LAKE LA 500 MGUU WA KUSHOTO BARCA IKIAMBULIA KIPIGO
Real Madrid, Granada,Atletico Madrid na Sevilla zote zipo na nafasi ya kushika uongozi wa ligi baada ya Barcelona kupoteza mechi yao dhidi ya Levante.
Barcelona imepokea kipigo cha goli 3 – 1 ugenini hata baada ya kufunga bao la kuongoza lililofungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati dakika ya 38 na kuandikisha goli lake la 500 kwa mguu wa kushoto akiwa klabuni hapo.

Dakika 7 ziliwatosha Levante kupindua matokeo kwa Jose Campana kusawazishia dakika ya 61 kabla ya Borja Mayoral aliyepo kwa mkopo tokea Real Madrid na Nemanja Radoja kuongeza mengine mawili dakika ya 63 na 68.
Matokeo haya yanaifanya Barcelona kuwa wamepoteza mechi tatu katika LaLiga msimu huu wakiwa na pointi 22 katika michezo 11 ambayo wameshacheza.