Raheem Sterling kamwaga wino Etihad
Kiungo Mshambuliaji wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica Raheem Sterling amefanikiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea na maisha katika jiji la Manchester kwa kuendelea kuichezea Manchester City, Sterling amesaini mkataba mpya wa kuendelea kucheza soka lake katika kikosi cha Pep Guardiola hadi mwaka 2023.
Mkataba huo wa miaka mitano utamfanya Raheem Sterling awe analipwa mshahara wa pound 300000 kwa wiki lakini ndio anakuwa mchezaji wa kiingereza anayelipwa mshahara mkubwa zaidi, Kocha Pep Guardiola ni moja kati ya watu waliopelekea mkataba kuongezwa kwa kiungo huyo kwani amewahi kukiri anamuona mbali katika soka.
Raheem Sterling mwenye umri wa miaka 23 baada ya kusaini mkataba huo ameonesha kushukuru na kufurahi kuendelea na maisha ya kucheza Etihad chini ya kocha Pep Guardiola ambaye anaamini kiungo huyo anaendelea kuimarika siku hadi siku.
Tukukumbushe tu Raheem Sterling ambaye alijiunga na Manchester City mwaka 2015 akitokea Liverpool, msimu huu katika Ligi Kuu Uingereza amepata nafasi ya kucheza michezo 9 sawa na dakika 772 akifunga magoli sita na kutoa pasi za mwisho za magoli 5, wastani ambao ni mzuri kwa mchezaji kulingana na idadi ya mechi alizocheza.