NI AFRIKA KUSINI DHIDI YA ENGLAND FAINALI YA KOMBE LA DUNIA RUGBY
Fainali za Rugby Kombe la Dunia zinamalizika leo jijini Yokohama nchini Japan kwa mechi ya fainali kati ya Afrika Kusini dhidi ya England fainali inayoonekana kuwa ya mvuto na kisasi kwa timu hizi zilizokutana katika hatua ya fainali ya michuano hii mwaka 2007 jijini Paris Ufaransa na Afrika kusini kufanikiwa kuibuka mabingwa
Baada ya kuifunga New Zealand katika nusu fainali sasa timu ya rugby ya Afrika Kusini maarufu kama ‘Springboks’ watakuwa kibaruani kuwania kushinda kombe hilo kwa mara ya tatu baada ya kuibuka mabingwa mwaka 1995 na mwaka 2007.

Springboks wanatarajia kuongeza nguvu kwenye kikosi chao kwa kupata huduma ya mchezaji wao mahiri Cheslin Kolbe anayetarajia kurudi dimbani leo hii baada ya kukosa nusu fainali kutokana na jeraha la goti.

England ambao wameingia fainali hizi kwa kuwatoa Wales wanatarajia kuingia dimbani bila mabadiliko yoyote kwenye kikosi huku wakiwa na imani ya kulipa kisasi cha mwaka 2007 na kufanikiwa twaa taji hilo kwa mara ya pili , mara ya kwanza ikiwa mwaka 2003 kipindi hicho mwana mfalme Harry akiwa na umri wa miaka 18.