PAWASSA KAMUITA DIDA TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI KUJIANDAA NA COPA DAR ES SALAAM
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni Boniface Pawassa amethibitisha kuwa amemuita kikosini golikipa wa zamani wa timu za Simba na Yanga Deogratus Munish ‘Dida’ kwa ajili ya Mashindano ya Copa Dar es salaam.
Dida ameitwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho kilichoanza mazoezi katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo inayotaraji kuchezwa katika fukwe za Coco kuanzia Desemba 20 hadi 26 2019.
Michuano ya Copa Dar es Salaam itashirikisha jumla ya timu za taifa nane ambazo ni Tanzania mwenyeji, Uganda, Libya, Shelisheli, Kenya, Malawi, Burundi na Msumbiji