SABABU ZA MKUDE KUKOSEKANA KATIKA MECHI ZA SIMBA DHIDI YA SINGIDA NA MWADUI FC
Afisa habari wa Simba SC Haji Manara amelitolea ufafanuzi swali la wengi kuhusiana na kukosekana kwa kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude katika michezo miwili ya Ligi Kuu.
Manara ameweka wazi kuwa Jonas Mkude amekosekana katika michezo ya Simba SC dhidi ya Singida United na Mwadui FC kwa sababu alikuwa anaumwa na ripoti ilitolewa na madaktari wa timu ya taifa kuwa hakuwa fiti.
“Jonas alikuwa anaumwa na alipewa mapumziko rasmi na uongozi wa klabu baada ya taarifa zake kutolewa na madaktari wa timu lakini karibuni atararudi hakuna tatizo lolote” alisema Haji kupitia Azam TV
Tukukumbushe Jonas Mkude alikuwa sehemu ya kikosi cha Taifa Stars kilichofuzu kwenda fainali za CHAN 2020 nchini Cameroon kwa kuifunga Sudan magoli 2-1 (agg 2-2) Oktoba 18 Khartoum Sudan na inadaiwa kuwa alipata majeraha madogo katika mchezo huo.