VIJANA WANNE WA KITANZANIA WENYE VIPAJI WATAENDA KUFANYA MAJARIBIO ULAYA MASHARIKI
Cambiasso Sports Management kwa kushirikiana na Rainbow Sports Alhamisi ya Oktoba 31 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ilihitimisha zoezi lake la kutafuta vipaji vya soka.
Cambiasso na Rainbow chini ya mkufunzi wa kusaka vipaji Alex Morfaw walifanikiwa kuchuja na kufanikiwa kupata watoto wanne katika kundi la watoto zaidi ya 1000 waliojitokeza katika usahili huo.

Watoto waliochaguliwa ni Samwel Jackson (Azam U20), Nasoro Saadun (Mtibwa U20), Teps Evans (Azam U20) na Abdulsatar Omary – Temeke na wataenda Ulaya kufanyiwa mafunzo mafupi na kutafutiwa academy.
Tukukumbushe tu ushirikiano wa Cambiasso Sports Management Sports na Rainbow ndio umefanikisha watanzania kwenda nje Abdallah Shaibu Ninja (LA Galaxy II), Ally Ng’anzi (Minnesota) na Yohana Mkomola anayecheza Arsenal Kiev ya Ukraine