Didier Drogba astaafu kwa majonzi
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba amemaliza vibaya maisha yake ya uchezaji wa mpira wa miguu baada ya timu yake ya Phoenix Rising kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Louisville kwenye fainali ya USL Cup huko nchini Marekani
Drogba ameiongoza Rising ambayo pia ni mmoja wa wamiliki kufika fainali kufika fainali ya mashindano hayo ya ligi daraja la pili nchini Marekani akifunga jumla ya goli tatu kwenye hatua ya mtoano.
Mchezaji huyo kutoka Ivory mwenye umri wa miaka 40 mwezi Machi mwaka huu alitangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu.
Kuachana na Chelsea, Drogba pia amezitumikia klabu za Le Mans, Marseille , Shanghai Shenhua , Galasaray na Montreal Impact.
Makombe na tuzo alizowahu kushinda Didier Drogba akiwa mchezaji.
1x Champions League
4x Premier League
4x FA Cup
3x League Cup
2x Community Shield
2x PL Golden Boot
1x Süper Lig
1x Turkish Cup
1x Turkish Super Cup
2x African POTY
1x Turkish POTY